Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s.) –ABNA– Watu wengi wasiofahamu kwa kina kanuni na mikakati ya vita walipoona kambi nyingi za kijeshi za Marekani zikizunguka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, walianza kuamini kwamba Iran ilikuwa imezingirwa kila upande na kwamba isingeweza kujinasua.
Baadhi yao walisema:
“Iran hapa hawezi kuchomoka! Kambi hizi za Marekani zilizoizunguka Iran kila upande zitaimaliza Iran.”
Hata hivyo, huenda walisahau - au hawakujua - kwamba Uislamu una mafundisho na maelekezo yanayowataka Waislamu kuwa na nguvu, maandalizi na uwezo wa kujilinda dhidi ya maadui.
Qur’ani Tukufu inaelekeza:
“Na waandalieni nguvu kama muwezavyo...”
(Qur’ani, Surah Al-Anfal 8:60)
Ujumbe wa aya hii unaonyesha umuhimu wa nguvu, maandalizi, tahadhari na uwezo wa kujilinda katika kukabiliana na maadui.
Kwa hiyo, wakati adui anatumia miaka mingi kujiandaa, kujenga vituo vya kijeshi, kukusanya silaha na kuzunguka nchi yako, si lazima ukubwa wa kambi zake uwe ishara kwamba adui huyo yuko salama au hawezi kushindwa.
Wakati mwingine, kambi nyingi za adui hazimaanishi kwamba adui yuko salama.
Huenda zikawa ni ramani ya maeneo ambayo adui mwenyewe amekuchorea ili uyafikie wakati wa mapambano.
Kwa mtazamo huu, kile ambacho baadhi ya watu walikiona kama kuzingirwa kwa Iran, wengine wanaweza kukitazama kama matokeo ya adui kujikusanya mwenyewe katika maeneo yaliyomuweka karibu zaidi na uwanja wa mapambano.
Hivyo, katika masuala ya ulinzi na usalama, si idadi ya kambi pekee inayopaswa kuangaliwa, bali pia maandalizi, uwezo wa kujibu, teknolojia, ujasusi, mshikamano na utayari wa taifa kukabiliana na changamoto.
Ujumbe mkuu ni kwamba adui anapojikusanya kwa miaka mingi karibu na mipaka yako, usidanganyike na wingi wa vituo vyake; muhimu ni kuwa tayari, kuwa na uwezo na kutambua kwamba nguvu ya kweli hujengwa kwa maandalizi ya muda mrefu.

Maoni yako